Thursday, 24 September 2015

BAADHI YA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI BAADA YA MATOKEO YA UTAFITI WA TWAWEZA


Ni leo tena nikivipitia vichwa vya habari kwa Magazeti mbalimbali ya hapa Nyumbani. Hii ni baada ya Utafiti wa kikundi flani kinachojiita TWAWEZA kutoa kile kinachokiita Utafiti .

Gazeti la Mwananchi

Gazeti hili limekuja na kichwa cha habari kikionyesha kuwa Utafiti wa Twaweza umetoka na kupondwa vibaya sana na Wananchi pamoja na Wasomi hapa Tanzania. Wakamaliza chini na Picha kuuuuuuubwaaaa ya Lowassa akifanya mkutano huko Masasi. (Ujumbe umeeleweka)

Gazeti la Nipashe

Gazeti hili limekuja na habari kubwa yenye kichwa cha habari, "Utafiti waipaisha ccm" ktk kushadidia habari hiyo chini yake limeandika "Wasomi na Wananchi wauponda vibaya sana" Chini wakamalizia na picha kuuuuubwaa ya mkutano wa Lowassa huko Masasi (Ujumbe umesomeka)

Gazeti la Tanzania Daima

Gazeti hili limekuja na habari kubwa yenye kichwa cha habari "Bao la Mkono, Twaweza watoa Utafiti kuibeba ccm, Wananchi wasomi Wauponda kila kona ya Nchi" Chini wakamalizia na Picha ya Mafuriko ya Lowassa huko Masasi (Ujumbe umeeleweka)

Gazeti la Raia Mwema

Gazeti hili lenyewe ndo halijataka hata kuripoti upuuzi wa Twaweza. Lenyewe limekuja na kichwa cha habari kilichoandikwa kwa ufupi sana, "MSHITUKO" Chini ya habari hiyo kuna picha kuuuuubwaa ya Lowassa akifanya mkutano wake huko Masasi wananchi wakiwa wamejazana kama mchanga wa bahari ya hindi. (Ujumbe pia umeeleweka)

NA BEN SAANANE

CCM wanaendelea kujiandalia njia ya kuelekea katika kaburi la Kisiasa na wamepita njia ile ile ambayo alipita Marehemu  PDP(Peoples Democratic Party) Cha Nigeria.

Chama cha PDP kilipokua kikipambana na Muungano wa UPinzani kupitia chama cha APC cha Mohammed Buhari nchini Nigeria walijikuta wakikosa ajenda ya kushawishi wananchi badala yake wakaamua kuwa waumini wa Siasa  za mitaroni kama kupanga matukio ya kuupaka matope upinzani,Kumtakia Kifo mgombea wa PDP n.k

Nguvu,Akili na Raslimali nyingi walizielekeza huko na matokeo yake walishindwa uchaguzi kisha baadae wakaanza kulaumiana na kujaribu kuvunja kamati kuu yao

Kwa Mbinu ileile CCM wamepanga mikakati inayofanana na ya PDP kwa matukio ya wiki

Hebu tazama mikakati yao ya ajabu ajabu

-Wiki ya Kwanza Lowassa alipohamia CHADEMA wao waliwekeza kwenye Tukio la Prof.Lipumba kujiuzulu

-Wiki ya Pili ambayo ilikua wiki ya Kwanza kwa Kampeni Tukio la Dr.Slaa kwao walilichukulia kama Mtaji kisha wakaendelea kupanga maana walinogewa.Ndipo walipoanza kupanga na kuelekeza smearing campaign yao kwa matukio kadhaa in series

-Wiki ya Tatu yaani wiki ya Pili ya Kampeni wakaibuka na siasa chafu za Udini huku Msemaji wa Chama akiwa kinara kabisa bila aibu kupotosha na kufanya siasa chafu za Udini ili kupandikiza chuki za kisiasa baina ya Ukristu/Ulutheri na Dini nyingine

-Wiki ya Nne(Wiki ya Tatu ya Kampeni) Wakaibuliwa  watu wawili (Moses na Letcia) NCCR-Mageuzi na kumshambulia Mbatia ,CHADEMA na UKAWA

-Wiki ya Tano(Ya nne kwa Kampeni) Ikaibuliwa TWAWEZA na Takwimu in reverse order.

-Leo Siku ya Idd ni Mapumziko, Tuna mkakati wa Wiki ijayo na mingine ukiwepo ule wa kumshawishi Kiongozi mmoja wa juu wa vyama vinavyounda UKAWA na ule wa kujaribu kuhonga baadhi ya MaofIsa na wakurugenzi  wa ngazi za juu wa vyama washirika wa UKAWA kufanya uasi

Viongozi wa Dini na makundi maalumu ya kijamii ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuandaliwa matukio hasi yatakayotumika kuchochea chuki dhidi ya Upinzani wiki nne zijazo kwa mujibu wa mkakati wao kama kilivyofanya chama tawala cha Nigeria PDP katika wiki za lala salama na vilevile walivyofanya KANU ya Kenya wiki ya Lala Salama

Tuendelee kubeba ajenda za wananchi na tuwe katika mood nzuri ya kuunda serikali mpya ya awamu ya Tano kutoka Upinzani kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru .

Tuanze awamu nyingine kwa ari zaidi na awamu ya kwanza kwetu ni fountain of inspiration baada ya kuvunja ngome za CCM katika awamu ya Kwanza.

Nilipokuwa Mtwara juzi nilipigwa Butwaa kwa Umati Wa Maelfu ya Wakazi wa Mtwara walioapa Uwanjani kulipiza kisasi  kupitia shahada zao juu ya dhuluma ya Utawala wa CCM katika sakata la Gesi

CCM sasa haina Ngome,Tumevunja Ngome zilizobaki za Lindi na Mtwara.

Unenguaji na push up za mgombea Urais Majukwaani umeshindwa kabisa kuwashawishi akina Mama wanaotembea kilometa nyingi kuteka maji,Wagonjwa wanaopata huduma mbovu. Pushup 3 za Magufuli zimeshindwa kabisa kuwashawishi vijana wasio na ajira na wanafunzi wanaokosa mikopo pamoja na walimu wanaoishi katika mazingira magumu. Hata kule Nigeria Mgombea Urais wa Chama Tawala Rais Jonathan aliJitahidi kupanda na nguo za michezo majukwani na kupiga sarakasi lakini alishindwa kurudisha ngome zilizotekwa na APC kwa ajenda

Tumefikia pale kilipofikia chama cha APC katika Wiki nne za Kampeni wakati CCM wanachanja mbuga kupita njia ya PDP iliyoshindwa na UKAWA ya Nigeria(APC)

Aluta Continua,Victory Ascerta.....

Ben Saanane

NGOME YA MWANZA YA NANI??? LOWASSA AU MAGUFULI??



Wakati kampeni zikiwa zimefikia katikati, vyama vya CCM na Chadema bado hazijajitosa mkoani

?

Dar es Salaam. Wakati kampeni zikiwa zimefikia katikati, vyama vya CCM na Chadema bado hazijajitosa mkoani Mwanza kufanya mikutano yake licha ya kupita mikoa inayouzunguka.

Mgombea wa CCM, John Magufuli jana alikuwa mkoani Geita baada ya kufanya kampeni Mkoa wa Kagera na anatarajiwa kuhamishia harakati zake mkoani Shinyanga.

Mgombea wa Chadema, ambaye pia anaungwa mkoano na vyama vingine vitatu vinavyounda Ukawa-NLD, CUF na NCCR Mageuzi-, jana alikuwa mkoani Lindi baada ya kufanya mikutano yake mkoani Mtwara na Dar es Salaam.

Tayari wagombea hao wawili, wanaochuana vikali wameshafanya mikutano ya kampeni katika mikoa inayopakana na Mwanza, lakini wanaonekana kutegeana au wameuweka kiporo mkoa huo, ambao una wapiga kura takriban milioni 1.4 kwa mujibu wa makadirio ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Mkoa wa Mwanza ambao ni kitovu cha shughuli za kiuchumi za mikoa ya Kanda ya Ziwa, unapakana na Kagera, unaokisiwa kuwa na wapigakura 217,390, Geita (808,337), Shinyanga (762,317), Simiyu (714,757) na Mara inayokisiwa kuwa na wapiga kura 834,580. Mkoa huo una majimbo ya Ukerewe, Nyamagana na Ilemela yaliyo chini ya Chadema, na Magu, Nyamagana, Buchosa, Misungwi na Sengerema yaliyo chini ya CCM.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa alifanya mikutano ya kampeni Mkoa wa Kagera, ambao uko Kaskazini Magharibi mwa Mwanza, Mara (Kaskazini Mashariki), Shinyanga, Simiyu na Geita iliyo upande wa Kusini.

Dk Magufuli amefanya mikutano ya kampeni kwenye mikoa hiyo pia akiuruka Mkoa wa Mwanza.

Walipoulizwa sababu za wagombea wao kuuweka kiporo Mkoa wa Mwanza, wasemaji wa vyama hivyo walisema wanafanya hivyo kwa kufuata ratiba na si kutegeana au kuuweka mkoa huo kiporo kwa malengo maalumu.

Mkurugenzi wa mawasiliano ya umma wa CCM, Godfrey Chongolo alisema jana kuwa wanafanya kampeni kulingana na ratiba ya Tume ya Uchaguzi (NEC), ambayo ilibadilika licha ya kuwa walipanga awali kufanya Mkoa wa Mwanza.

?Unajua NEC ndio wanaopanga ratiba. Vyama vyote vimepangiwa ratiba na kila mahali kwa tarehe zake za kampeni, sasa huwezi kwenda nje ya hapo utakuwa unakiuka taratibu,? alisema Chongolo.

Hata hivyo, alisema kuwa watafanya kampeni Geita na leo Alhamisi wataanzia Kahama na baadaye Shinyanga mjini kuhitimisha kampeni za Kanda ya Ziwa.

Alisema baada ya ratiba hiyo, Dk Magufuli na timu yake watarudi Dar es Salaam kabla ya kuendelea na ziara kama hiyo visiwani Zanzibar.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, ofisa habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema kuwa Ukawa wanafuata ratiba ya NEC na hawawezi kufanya kampeni nje ya ratiba ya chombo hicho cha uchaguzi

?Hatuwezi kujifanyia kampeni tunavyotaka, NEC wamepanga hivyo. Tulipeleka mapendekezo, lakini NEC wakaja na ratiba nzima ya kampeni, na hata ukiangalia, kila mahali tunaacha baadhi ya maeneo ya kuja kumalizia.

?Huu ni mpango mkakati vilevile, umetusaidia, kwanza mpango wetu ni kuacha kila kanda mkoa mmoja au eneo moja kwa ajili ya kuja kuhitimisha, hatutaki kuondoka moja kwa moja,? alisema.

Alisema kuwa Ukawa imejipanga tangu uzinduzi ndiyo maana baada ya uzinduzi moja kwa moja walikwenda Nyanda za Juu Kusini na kuendelea na ratiba.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, vyama vinatakiwa kupeleka NEC mapendekezo ya ratiba za shughuli zao za kampeni na Tume huangalia ratiba za vyama vyote na kutoa ya mwisho ambayo inaondoa migongano kwa vyama.

Wagombea hao pia wamegusa sehemu ndogo ya mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, inayojumuisha mikoa ya Mbeya, Katavi, Rukwa, Iringa na Njombe, lakini ukiondoa CCM wameepuka kuingia Jiji la Mbeya, ambalo linakisiwa kuwa na wapigakura wapatao milioni 1.47. Mikoa hiyo inakisiwa kuwa na jumla ya wapiga kura milioni 3.1.

Mbali na mikoa hiyo miwili yenye watu wengi, wagombea hao wawili wamefanya mikutano mkoani Tanga na kuacha kiporo mikoa mingine ya kaskazini, ambayo ni Kilimanjaro, Manyara na Arusha.

Mikoa ya kaskazini ina jumla ya wapigakura milioni 3.8 na vyama hivyo vina mpambano mkali kwenye majimbo.

Mpaka sasa, NEC imekwishaandikisha watu 24,252,927 kwa mujibu wa takwimu za makadirio zilizotolewa na NBS Julai 17, 2015 ikionyesha kukamilika katika mikoa 17

Kati ya hao, mikoa mingi ikiwemo Mwanza na Dar es Salaam ndiyo yenye watu wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 4.4. Mkoa wa Mwanza una watu milioni 1.4 na Dar es Salaam ni milioni tatu.

Mgombea wa CCM, Dk Magufuli bado ameweka akiba ya kampeni kwa mikoa hiyo wakati Lowassa ameshagusa sehemu ya Dar es Salaam katika maeneo ya Bunju, Tegeta, Chanika, Kigamboni na Mbagala.

Saturday, 5 September 2015

ALICHO KISEMA BEN SAANANE

Naandika kuweka sawa taarifa zilizojaa upotoshaji ambazo zimekua zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na pia kwenye vyumba vya habari tangu jana usiku . Sitawajibia wengine.

Kwanza,Iliandikwa kwamba mimi Ben Saanane na baadhi ya maofisa wa CHADEMA makao Makuu na wakurugenzi wa chama cha CUF tumeandaa mkutano na waandishi wa Habari Serena Hotel siku ya Ijumaa Tarehe 04/09/2015 Saa saba Mchana

Pili ,Taarifa hiyo ikaibua mijadala JamiiForums na mitandao mingine ya kijamii ikiambatana na tuhuma kuwa tunaungana na Dr.Slaa na Prof.Lipumba na kuwa tumehongwa

Tatu,Zikaibuliwa Tuhuma kuwa sijawahi kushiriki mijadala ya kukijenga chama changu tangu Lowassa alipohamia CHADEMA na kuwa Mgombea Urais badala ya Dr.Slaa.

Nne,Zikaibuliwa tuhuma kuwa nipo vitani dhidi ya chama chetu na watu hao kurejea sakata la kikanuni ndani ya Chama kati ya aliyekua Naibu Katibu Mkuu Ndugu Zitto,Mjumbe wa Kamati Kuu Dr.Kitila Mkumbo dhidi ya Chama na Ushiriki wangu katika sakata lile.

Naomba nifafanue kulingana na mahitaji ya wakati kisha nitaweka akiba baadhi ya masuala.kwa maslahi ya Harakati za Mageuzi,Nchi Yangu,Chama Changu,Harakati zangu kisiasa na pia mustakabali mwema kwa wale ninaoheshimu mchango wao kwa Taifa letu.

Kwanza, Sijaandaa mkutano wowote na waandishi wa Habari na sina sababu ya kufanya hivyo hivi sasa.

Pili,Ni kweli sijaandika kwa kiwango ambacho pengine kingeridhisha baadhi ya watu .

Sikufanya hivyo kwa bahati mbaya (yaani kutokuandika) bali kwa malengo Mahsusi kitaaluma na kisiasa.

Chama Chetu na umoja wetu -UKAWA kimekua katika changamoto ya kisiasa kufuatia msimamo wa katibu Mkuu Dr.Slaa  na pia msimamo wa Mwenyekiti Mwenza Prof.Lipumba.

Jitihada za kisiasa na  kidiplomasia zilifanyika kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha hatumuachi mtu hata mmoja nyuma katika safari yetu hii ya Mwisho ya vuguvugu la mabadiliko

Katika jitihada za kidiplomasia na kisiasa,nilihusika moja kwa moja.

Sikuona mantiki yoyote kuandika kutokana na kuwa mojawapo wa kanuni za msingi kabisa katika majadiliano ya kidiplomasia ni kuhakikishwa kuwa washiriki wa meza ya mazungumzo hawaonyeshi misimamo ya kuegemea upande fulani ikiwa kweli wana lengo la dhati la kushawishi pande zote au upande mwingine ukubaliane kutokubaliana

Ni lazima kuwe na mazingira ya imani(confidence atmosphere).

Kutokuandika ndio "Confidence Atmosphere" yenyewe ambayo katika meza ya mazungumzo/majadiliano (Negotiation Table) ni silaha mahsusi kwa wanataaluma,wataalamu wa Diplomasia na wanasiasa Makini huitumia kuepusha mifarakano na kuafikiana.

Haya ni masuala ambayo nimejifunza sana kupitia taaluma yangu ya Uhusiano wa Kimataifa na diplomasia,Pia kiutendaji na malezi ya kisiasa na kiuongozi kutoka kwa baadhi ya viongozi .Hivyo kumshambulia Dr.Slaa ingekua najiweka katika nafasi ya  kichocheo(Catalyst position) katika migongano.

Vilevile,Habari zimesambazwa kuwa simshambulii Dr.Slaa tangu juzi.

Ni Kweli sioni Sababu ya kumshambulia Dr.Slaa .Sifuati Mkumbo,Sifuati mihemko na wala sijawahi kujipendekeza kwa yeyote na sina mpango huo.Nafuata maadili ya kitaaluma kutoka kwa walimu wangu,uzoefu wa kiweledi kutoka katika Mashirika na taasisi mbalimbali ikiwemo malezi ya kiuongozi ndani ya chama changu


Sijawahi kufundishwa kumshambulia mtu hasa bosi wangu wa Zamani au taasisi niliyokua nikiifanyia kazi unless nitoe ufafanuzi kwa suala linalogusa moja kwa moja idara yangu au mimi binafsi.Chama au UKAWA kina wasemaji wake,wanatosha.

Kwangu yeye anaendelea kubakia kuwa Kiongozi wa mfano,Boss wa mfano ambaye Msomi yeyote angejivunia na kujisikia huru kufanya nae kazi.Hakika nitamkosa sana kiofisi

Tarehe 28 July,2012  siku ya Jumamosi nikiwa nyumbani kwake , Dr.Slaa  mwenyewe  aliwahi kuniambia "Dont Support Slaa,You Should Support and fight for the right Cause".Niliheshimu na naendelea kusimamia hilo hata kama kuna mahali ameteleza kama bindamu.Nitachukua yote mazuri.Mara ya Mwisho (siku chache zilizopita) nilipowasiliana nae alinisihi niheshimu maamuzi yake kama ninavyotarajia aheshimu ya kwangu.Nilifanya hivyo.

Nitaendelea kumuheshimu Dr.Slaa kama kiongozi aliyenilea kiuongozi na kuboresha weledi wangu kiutendaji kwa kuwa ana mchango mkubwa kwangu katika malezi ya kiuongozi na sitasita kumfuata na kumuomba ushauri kama nifanyavyo kwa Dr.Salim Ahmed Salim, Prof.Kitila Mkumbo,Kaka yangu Tundu Lissu na Rafiki yangu Halima Mdee hata Ndugu Zitto Kabwe ambae tulikuja kuunganishwa pamoja tena katika vita ya ESCROW na wengineo.


Sioni mantiki ya mimi kumshambulia Dr.Slaa kwa kuwa pia mamlaka zinazohusika zinaweza kujibu pale inapoonekana kuna ulazima au pale ambapo nafasi yangu binafsi au kiutendaji imeguswa moja kwa moja  hasa idara yangu ya Sera,Ilani na Utafiti.Hapo nitafafanua

Tatu,Kwa sasa najielekeza kukisaidia chama changu kushinda Uchaguzi. Najielekeza kufafanua Ilani ya chama chetu kwa wananchi na pia kushiriki katika tafiti na kufikia maamuzi ya kimkakati ili chama chetu kipate ushindi Mkubwa.

Ni lazima tuheshimu maamuzi ya kamati kuu,Baraza kuu na mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba.Ndio malezi niliyolelewa kiuongozi katika dhana ya "team work" na "Collective Responsibility"

Chama chetu kimewahi kupita katika changamoto kubwa na upinzani umetikiswa sana lakini naamini huu ndio muda wetu.Wazungu husema "This is our moment".


Nawaasa vijana wenzangu tuzingatie sana muda uliobaki kabla ya Oktoba 25,2015

Na zaidi tumuombe Mwenyezi Mungu atuvushe katika kipindi hiki chenye Changamoto kubwa ,tusiache kuombeana katika hali yoyote ile

Aluta Continua,Victory Ascerta....
Ben Saanane

ALICHO KISEMA RAIS WA MUCE JUU YA TUHUMA ZA LOWASSA

Nanukuu.

"Lowasa nimsamehe kwa kosa gani?

Ngoja niwakumbusheni kidogo, Siku zile kashfa ya Richmond imezuka na Lowasa amejiuzulu mimi binafsi mbali ya kuwa Rais wa MUCE nilikuwa Kamishna wa TAHLISO.Tulifanya kikao chetu Arusha na kuamua kuandamana nchi Nzima ktk miji ya kivyuo yaani IRINGA, MOROGORO, MBEYA, DODOMA, DAR, MOSHI, ARUSHA, NA MWANZA. Mimi niliongoza maanda. ano ya Mbeya na Rais wa Muhumbili wakati huo alikuja kuongoza ya Iringa. Katika maandamano yetu tulidai mambo mawili, Mosi waliopiga Richmond wapelekwe mahakamani, Pili tulitaka ikithibitika mali zao zitaifishwe kufidia upotevu na kuboresha huduma za umeme. Nakumbuka tulisikika sana ktk medea na ilikuwa ni mara ya kwanza ktk nyakati zetu Wanazuoni kuandamana na kutishia migomo kwa maslahi ya umma  co matumbo yetu kama ilivo ada. Nini kilitokea, Rais alikuja publicaly na kumsemea edo kuwa alikuwa kapata ajali ya kisiasa na si mwizi, Rais alienda kwa kampeni Monduli uchaguzi wa 2010 akadai edo ni mtu safi mchapakazi, Kinana akiwa ktk ziara zake akasema Lowasa safi Nyarando Mzigo, Walojiita makamanda wa kupinga ufisadi ktk mradi wa Mwakyembe kama Lugola, Ole sendeka,Serukamba, nawengineo wakageuka na kuwa kambi Lowasa ktk safari yake ya kutaka urais. Upande wa pili serikali hiyohiyo nje ya Lowasa ikaibariki mitambo ya Richmond  ikawa Dowans na hatimaye Symbion iendelee kutupigia kazi nchini, nakumbuka safari hii hata alokuwa kiongozi wangu Zito alisema hapa hakuna shida itumike coz Ri hmond ni mchezo ulicgezwa na Ma ccm ili kumalizana kisiasa wao kwa wao.Hayo yakiendelea Kikwete akawapeleka Mahakamani mafisadi papa kama Mramba, Yona na Mgonja. Wawili wamefungwa, Ivi kama mawaziri hawa wako jela kwa ufisadi Lowasa anatafuta nn nje leo? Tena hata kesi tu hana?Najiuliza Lowasa leo kahama chama na kwa hulka ya TANZANIA sote tunajua wezi, wachafu hata majambazi hujibanza ccm ili wasishtakiwe au wahurumiwe maovu yao, lakini Edo kawaambia tena na tena Serikali safari hii akiwa nje ya ccm kuwa anayenituhumu kwa rushwa anipeleke mahakamani wapi badala yake wanakuja na porojo kwa kumpatia nyaraka Mzee Slaa akidai eti mkizitaka hizi mwende ikulu? Yeye ikulu wamempa za nn badala ya kupeleka mtuhumiwa mahakamani?Kwa mtu mwenye akili timamu zinazojitegemea kama mimi nimekataa, Sitadanganywa kamwe, Lowasa kwa muktadha wa Richmond  sio fisadi kabisa, Anaedai namsafisha hajui, Wachafu ndo husafishwa,Kwa kuwa naamini tuna haja ya kubadili mfumo wa utawala ili kubeba agenda zetu za mabadiliko kama katiba ya wananchi, kwa kuwa edo kio gozi mzoefu anayependwa ameamua kuwa upande wetu, basi atapewa kura c yangu tu bali na mamilioni ya watazania."