Thursday, 24 September 2015

NA BEN SAANANE

CCM wanaendelea kujiandalia njia ya kuelekea katika kaburi la Kisiasa na wamepita njia ile ile ambayo alipita Marehemu  PDP(Peoples Democratic Party) Cha Nigeria.

Chama cha PDP kilipokua kikipambana na Muungano wa UPinzani kupitia chama cha APC cha Mohammed Buhari nchini Nigeria walijikuta wakikosa ajenda ya kushawishi wananchi badala yake wakaamua kuwa waumini wa Siasa  za mitaroni kama kupanga matukio ya kuupaka matope upinzani,Kumtakia Kifo mgombea wa PDP n.k

Nguvu,Akili na Raslimali nyingi walizielekeza huko na matokeo yake walishindwa uchaguzi kisha baadae wakaanza kulaumiana na kujaribu kuvunja kamati kuu yao

Kwa Mbinu ileile CCM wamepanga mikakati inayofanana na ya PDP kwa matukio ya wiki

Hebu tazama mikakati yao ya ajabu ajabu

-Wiki ya Kwanza Lowassa alipohamia CHADEMA wao waliwekeza kwenye Tukio la Prof.Lipumba kujiuzulu

-Wiki ya Pili ambayo ilikua wiki ya Kwanza kwa Kampeni Tukio la Dr.Slaa kwao walilichukulia kama Mtaji kisha wakaendelea kupanga maana walinogewa.Ndipo walipoanza kupanga na kuelekeza smearing campaign yao kwa matukio kadhaa in series

-Wiki ya Tatu yaani wiki ya Pili ya Kampeni wakaibuka na siasa chafu za Udini huku Msemaji wa Chama akiwa kinara kabisa bila aibu kupotosha na kufanya siasa chafu za Udini ili kupandikiza chuki za kisiasa baina ya Ukristu/Ulutheri na Dini nyingine

-Wiki ya Nne(Wiki ya Tatu ya Kampeni) Wakaibuliwa  watu wawili (Moses na Letcia) NCCR-Mageuzi na kumshambulia Mbatia ,CHADEMA na UKAWA

-Wiki ya Tano(Ya nne kwa Kampeni) Ikaibuliwa TWAWEZA na Takwimu in reverse order.

-Leo Siku ya Idd ni Mapumziko, Tuna mkakati wa Wiki ijayo na mingine ukiwepo ule wa kumshawishi Kiongozi mmoja wa juu wa vyama vinavyounda UKAWA na ule wa kujaribu kuhonga baadhi ya MaofIsa na wakurugenzi  wa ngazi za juu wa vyama washirika wa UKAWA kufanya uasi

Viongozi wa Dini na makundi maalumu ya kijamii ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuandaliwa matukio hasi yatakayotumika kuchochea chuki dhidi ya Upinzani wiki nne zijazo kwa mujibu wa mkakati wao kama kilivyofanya chama tawala cha Nigeria PDP katika wiki za lala salama na vilevile walivyofanya KANU ya Kenya wiki ya Lala Salama

Tuendelee kubeba ajenda za wananchi na tuwe katika mood nzuri ya kuunda serikali mpya ya awamu ya Tano kutoka Upinzani kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru .

Tuanze awamu nyingine kwa ari zaidi na awamu ya kwanza kwetu ni fountain of inspiration baada ya kuvunja ngome za CCM katika awamu ya Kwanza.

Nilipokuwa Mtwara juzi nilipigwa Butwaa kwa Umati Wa Maelfu ya Wakazi wa Mtwara walioapa Uwanjani kulipiza kisasi  kupitia shahada zao juu ya dhuluma ya Utawala wa CCM katika sakata la Gesi

CCM sasa haina Ngome,Tumevunja Ngome zilizobaki za Lindi na Mtwara.

Unenguaji na push up za mgombea Urais Majukwaani umeshindwa kabisa kuwashawishi akina Mama wanaotembea kilometa nyingi kuteka maji,Wagonjwa wanaopata huduma mbovu. Pushup 3 za Magufuli zimeshindwa kabisa kuwashawishi vijana wasio na ajira na wanafunzi wanaokosa mikopo pamoja na walimu wanaoishi katika mazingira magumu. Hata kule Nigeria Mgombea Urais wa Chama Tawala Rais Jonathan aliJitahidi kupanda na nguo za michezo majukwani na kupiga sarakasi lakini alishindwa kurudisha ngome zilizotekwa na APC kwa ajenda

Tumefikia pale kilipofikia chama cha APC katika Wiki nne za Kampeni wakati CCM wanachanja mbuga kupita njia ya PDP iliyoshindwa na UKAWA ya Nigeria(APC)

Aluta Continua,Victory Ascerta.....

Ben Saanane

No comments:

Post a Comment