Saturday, 5 September 2015

ALICHO KISEMA BEN SAANANE

Naandika kuweka sawa taarifa zilizojaa upotoshaji ambazo zimekua zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na pia kwenye vyumba vya habari tangu jana usiku . Sitawajibia wengine.

Kwanza,Iliandikwa kwamba mimi Ben Saanane na baadhi ya maofisa wa CHADEMA makao Makuu na wakurugenzi wa chama cha CUF tumeandaa mkutano na waandishi wa Habari Serena Hotel siku ya Ijumaa Tarehe 04/09/2015 Saa saba Mchana

Pili ,Taarifa hiyo ikaibua mijadala JamiiForums na mitandao mingine ya kijamii ikiambatana na tuhuma kuwa tunaungana na Dr.Slaa na Prof.Lipumba na kuwa tumehongwa

Tatu,Zikaibuliwa Tuhuma kuwa sijawahi kushiriki mijadala ya kukijenga chama changu tangu Lowassa alipohamia CHADEMA na kuwa Mgombea Urais badala ya Dr.Slaa.

Nne,Zikaibuliwa tuhuma kuwa nipo vitani dhidi ya chama chetu na watu hao kurejea sakata la kikanuni ndani ya Chama kati ya aliyekua Naibu Katibu Mkuu Ndugu Zitto,Mjumbe wa Kamati Kuu Dr.Kitila Mkumbo dhidi ya Chama na Ushiriki wangu katika sakata lile.

Naomba nifafanue kulingana na mahitaji ya wakati kisha nitaweka akiba baadhi ya masuala.kwa maslahi ya Harakati za Mageuzi,Nchi Yangu,Chama Changu,Harakati zangu kisiasa na pia mustakabali mwema kwa wale ninaoheshimu mchango wao kwa Taifa letu.

Kwanza, Sijaandaa mkutano wowote na waandishi wa Habari na sina sababu ya kufanya hivyo hivi sasa.

Pili,Ni kweli sijaandika kwa kiwango ambacho pengine kingeridhisha baadhi ya watu .

Sikufanya hivyo kwa bahati mbaya (yaani kutokuandika) bali kwa malengo Mahsusi kitaaluma na kisiasa.

Chama Chetu na umoja wetu -UKAWA kimekua katika changamoto ya kisiasa kufuatia msimamo wa katibu Mkuu Dr.Slaa  na pia msimamo wa Mwenyekiti Mwenza Prof.Lipumba.

Jitihada za kisiasa na  kidiplomasia zilifanyika kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha hatumuachi mtu hata mmoja nyuma katika safari yetu hii ya Mwisho ya vuguvugu la mabadiliko

Katika jitihada za kidiplomasia na kisiasa,nilihusika moja kwa moja.

Sikuona mantiki yoyote kuandika kutokana na kuwa mojawapo wa kanuni za msingi kabisa katika majadiliano ya kidiplomasia ni kuhakikishwa kuwa washiriki wa meza ya mazungumzo hawaonyeshi misimamo ya kuegemea upande fulani ikiwa kweli wana lengo la dhati la kushawishi pande zote au upande mwingine ukubaliane kutokubaliana

Ni lazima kuwe na mazingira ya imani(confidence atmosphere).

Kutokuandika ndio "Confidence Atmosphere" yenyewe ambayo katika meza ya mazungumzo/majadiliano (Negotiation Table) ni silaha mahsusi kwa wanataaluma,wataalamu wa Diplomasia na wanasiasa Makini huitumia kuepusha mifarakano na kuafikiana.

Haya ni masuala ambayo nimejifunza sana kupitia taaluma yangu ya Uhusiano wa Kimataifa na diplomasia,Pia kiutendaji na malezi ya kisiasa na kiuongozi kutoka kwa baadhi ya viongozi .Hivyo kumshambulia Dr.Slaa ingekua najiweka katika nafasi ya  kichocheo(Catalyst position) katika migongano.

Vilevile,Habari zimesambazwa kuwa simshambulii Dr.Slaa tangu juzi.

Ni Kweli sioni Sababu ya kumshambulia Dr.Slaa .Sifuati Mkumbo,Sifuati mihemko na wala sijawahi kujipendekeza kwa yeyote na sina mpango huo.Nafuata maadili ya kitaaluma kutoka kwa walimu wangu,uzoefu wa kiweledi kutoka katika Mashirika na taasisi mbalimbali ikiwemo malezi ya kiuongozi ndani ya chama changu


Sijawahi kufundishwa kumshambulia mtu hasa bosi wangu wa Zamani au taasisi niliyokua nikiifanyia kazi unless nitoe ufafanuzi kwa suala linalogusa moja kwa moja idara yangu au mimi binafsi.Chama au UKAWA kina wasemaji wake,wanatosha.

Kwangu yeye anaendelea kubakia kuwa Kiongozi wa mfano,Boss wa mfano ambaye Msomi yeyote angejivunia na kujisikia huru kufanya nae kazi.Hakika nitamkosa sana kiofisi

Tarehe 28 July,2012  siku ya Jumamosi nikiwa nyumbani kwake , Dr.Slaa  mwenyewe  aliwahi kuniambia "Dont Support Slaa,You Should Support and fight for the right Cause".Niliheshimu na naendelea kusimamia hilo hata kama kuna mahali ameteleza kama bindamu.Nitachukua yote mazuri.Mara ya Mwisho (siku chache zilizopita) nilipowasiliana nae alinisihi niheshimu maamuzi yake kama ninavyotarajia aheshimu ya kwangu.Nilifanya hivyo.

Nitaendelea kumuheshimu Dr.Slaa kama kiongozi aliyenilea kiuongozi na kuboresha weledi wangu kiutendaji kwa kuwa ana mchango mkubwa kwangu katika malezi ya kiuongozi na sitasita kumfuata na kumuomba ushauri kama nifanyavyo kwa Dr.Salim Ahmed Salim, Prof.Kitila Mkumbo,Kaka yangu Tundu Lissu na Rafiki yangu Halima Mdee hata Ndugu Zitto Kabwe ambae tulikuja kuunganishwa pamoja tena katika vita ya ESCROW na wengineo.


Sioni mantiki ya mimi kumshambulia Dr.Slaa kwa kuwa pia mamlaka zinazohusika zinaweza kujibu pale inapoonekana kuna ulazima au pale ambapo nafasi yangu binafsi au kiutendaji imeguswa moja kwa moja  hasa idara yangu ya Sera,Ilani na Utafiti.Hapo nitafafanua

Tatu,Kwa sasa najielekeza kukisaidia chama changu kushinda Uchaguzi. Najielekeza kufafanua Ilani ya chama chetu kwa wananchi na pia kushiriki katika tafiti na kufikia maamuzi ya kimkakati ili chama chetu kipate ushindi Mkubwa.

Ni lazima tuheshimu maamuzi ya kamati kuu,Baraza kuu na mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba.Ndio malezi niliyolelewa kiuongozi katika dhana ya "team work" na "Collective Responsibility"

Chama chetu kimewahi kupita katika changamoto kubwa na upinzani umetikiswa sana lakini naamini huu ndio muda wetu.Wazungu husema "This is our moment".


Nawaasa vijana wenzangu tuzingatie sana muda uliobaki kabla ya Oktoba 25,2015

Na zaidi tumuombe Mwenyezi Mungu atuvushe katika kipindi hiki chenye Changamoto kubwa ,tusiache kuombeana katika hali yoyote ile

Aluta Continua,Victory Ascerta....
Ben Saanane

No comments:

Post a Comment